Wasimamizi Wa Idara Ndani Ya Kanisa
- Idara ya Vijana [Alex Mkandawile, +255713969152]
- Idara ya Wakinababa [Geofrey Mwesiga, +255742437602]
- Idara ya Wakinamama [Mch. Sophia Sarungi ,+255657483150]
- Idara ya Uinjilist [Obedi Mwakapiki, +255685316601]
- Idara ya watoto
: IDARA MBALIMBALI NDANI YA GROWING MISSION CHURCH.
➢ Kanisa hili litakuwa na idara mbalimbali kama ifuatavyo:
IDARA YA WAMAMA
➢ Idara hii itajulikana kwa jina la Wanawake Jeshi Kubwa kwa kifupi chake W.J.K.
Kazi ya idara ya wamama:
1. Ni kusimamia malengo ya idara ya wanawake
2. kuona kwamba akina mama wanaongozwa katika misingi ya kiroho
pamoja na kutunza watoto wao vizuri.
3. Kuhakikisha kwamba wakina mama nao wanajihusisha katika kueneza
kazi ya Mungu.
16
IDARA YA VIJANA (CAIM)
➢ Idara hii itajulikana kwa jina la Mabalozi wa Huduma ya Kristo (Christ
Ambassadors in Mission) kwa kifupi MHK ( CAIM)
Kazi ya Idara ya vijana (CAIM)
1. Kuwasaidia vijana kwa njia ya mafundisho ili wakue katika hali ya kumcha
Mungu
2. Kuwasaidia vijana kusudi wajue jinsi ya kushuhudia Neno la Mungu
mitaani/sokoni/Hospitalini/Magerezani/shuleni/na mikutano ya
hadhara.
3. Kuwafanya vijana wajue jinsi ya kutegemeza makanisa/shule/za Biblia
kwa fedha zao na maombi yao.
4. Kuwaunganisha vijana wa kanisa letu nchi nzima na kushirikiana na vijana
wenye imani sawa na yetu ulimwenguni.
5. Kuwasaidia vijana kwa hali na mali wakati wanapofikia kuoa au kuolewa
IDARA YA WABABA (WWN )
Idara hii itajulikana kwa jina la Wababa ni Watendaji wa Neno
Kazi ya idara ya wababa
1. Ni kusimamia malengo ya idara ya wababa
2. kuona kwamba akina baba wanaongozwa katika misingi ya kiroho
pamoja na kutunza familia zao vizuri, yaani mke na watoto.
3. Kuhakikisha kwamba wakina baba nao wanajihusisha katika kueneza
kazi ya Mungu, kama Wababa watendaji wa Neno lilivyo.
IDARA YA WATOTO ( HUWK )
Hii ni idara muhimu sawa na idara nyingine katika kanisa yenye lengo la kutoa
elimu ya Biblia kanisani kwa kila mkristo. Kwa kifupi itaitwa Huduma ya Uangalizi
wa Watoto wa Kikristo (HUWK)
Kazi yake:- ( Mithali 22:6 na Mithali 4:13)
1. Ni kufundisha Sunday school ukizingatia sana Neno la Mungu kuanzia
Agano la kale na Agano jipya ili kuhakikisha kwamba Biblia nzima
inafundishwa kwa wanafunzi wa rika zote (kanisa).
17
2. Waalimu wa shule hii ya Jumapili lazima wawe ni wakristo wanaoelewa
vizuri Neno la Mungu na wawe na uwezo wa kufundisha wengine.
3. Mchungaji au Baraza la wazee wahakikishe kuwa walimu hao wana
maisha safi ya kiroho na elimu inayokubalika na nchi yetu. Isaya 52:11c
0 Comments